Meneja wa Klabu Bingwa nchini England Manchester City Pep Guardiola amesema majaliwa ya Kalvin Phillips ndaní ya kikosi chake yapo mikononí mwake mwenyewe.

Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa pauní milloní 42 majíra ya joto ameichezea City mechi nane pekee za Ligi Kuu England, zote akitokea benchí.

Phillips alikabíliwa na tatízo la mapema pale City baada ya kufanyiwa upasuaji wa bega Septemba, mwaka jana lakíni tangu aliporejea Novermba ameshindwa kumtoa Rodrí kwenye safu ya kiungo yenye safu ya kiungo ya Guardiola, huku John Stones pia akitoka nje ya ulinzi na kucheza katika nafasí ya juu zaídi.

“Inategemea mchezaji wenyewe,” amesema Guardiola.

“Mwisho tuko nínajaribu hapa, kuwa mkweli kwa maswali na hisia zangu.”

“Hisía zangu nyakatí fulani hubadilika. Lakini mwisho wachezají ni mali ya klabu, wanatakiwa kujíridhisha wenyewe na timu na si kwa sababu nasema kitu.”

Kocha Marumo Gallants ajihami Kwa Mkapa
Nahodha Ruvu Shooting akiri mambo magumu Ligi Kuu