Rais wa Marekani Donald Trump ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini Uingereza ziara ambayo anaifanya wakati taifa hilo likijaribu kupata ushirikiano wa umoja wa Ulaya kuhusu mpango wake wa kujitoa BREXIT.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Uingereza na Marekani vimeripoti kuwa ziara hiyo imezua gumzo baada ya matamshi ya Rais Trump ya hivi karibuni ambyo alisema wazi kuwa anamuunga mkono kiongozi wa upinzani Nigel Farage na kwamba angepaswa kujumuishwa kwenye mazungumzo  ya BREXIT.

Kabla ya kuwasili London kutoka washington DC kulikuwa na fununu kuwa  wanaharakati wamepanga kufanya maandamano  makubwa  jijini Londoni na miji mingine mikubwa Uingereza kupinga ziara hiyo.

Kwenye mahojiano na gazeti la The Sun mbali na kumuunga mkono Farage, Raisi Trump amesema kuwa angependela  kuona Boris Johnson anateuliwa kuwa waziri mkuu ajae.

Hata hivyo Uingereza inatarajiwa kuwa na Waziri mkuu mpya hivi kribuni baada ya Theresa May kutangaza kuwa atajiuzulu  juni 7 mwaka huu.

Mara baad ya kuwasili jijini Londoni taarifa zilisema kuwa Rais Trump aliandaliwa dhifa malumu na Malkia Elizabeth  wa pili wa Uingereza ambapo ameambatana na mke wake Melania Trump.

 

Mlinzi aliye muua mwanafunzi ahukumiwa kunyongwa
Watanzania waamka kwenye kilimo biashara