Habari zinazomhusu mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, Ilkay Gundogan zinatatanisha.

Mwanzoni mwa mwezi huu ilidaiwa kwamba mchezaji huyo hakusaini mkataba wa muda mrefu na klabu yake ya Borussia Dortmund kwa lengo la kutaka kuhamia klabu nyingine katika ligi ya Bundesliga.

Hata hivyo, habari mpya ni kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa katika klabu ya Borussia Dortmund tangu mwaka 2011, anataka kumfuata kocha wake aliyekuwanae kwa muda mrefu, Jurgen Klopp ambaye sasa anakinoa kikosi cha Liverpool.

Gundogan ameliambia gazeti la Bild, hajafanya uamuzi wowote na lazima atasaini kila kitu kwa sababu urefu ya taaluma ya mtu una ukomo.

Ameongeza kuwa kila kitu kingali wazi na kuwa mkataba wake ujao utakuwa mrefu na sio wa mwaka mmoja tu.

Amesema kwamba anataka kulinda kiwango chake, lakini haoni kwamba kuna timu ambayo inaweza kusaidia kikosi chake zaidi ya Liverpool kwa sababu katika kikosi hicho kuna mtu ambaye anajua kwamba anamfaa.

Na wala hafichi, anamtaja mtu huyo kuwa ni Klopp ambaye anadai kuwa alikuwa nae katika kikosi hicho kwa kiwango cha mtu na kaka yake na alimsaidia sana.

“Alikuwa kama kaka au baba yangu hapa, nikienda Uingereza kwa vyovyote vile sitakwenda Arsenal au Man United, sitakwenda Chelsea au Man City, nitakwenda Liverpool kwa sababu ya Klopp,” alisema.

 

Membe amkosoa Magufuli kuhusu Kubana Matumizi, Safari za nje
Luis Suarez Ampuuza Andon Zubizarreta