Polisi Mkoani Mwanza, imeanza msako wa kuwatafuta wahalifu waliojichukulia sheria mkononi kwa kuwashambulia kwa mawe na silaha za jadi Nna kuwauwa watu wawili wakiwatuhumu kuiba gunia moja la mpunga.

Akiongea na vyombo vya Habari hii leo Oktoba 3, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani wa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa amesema tukio hilo lilitokea Oktoba 30, 2023 majira ya saa 11:30 jioni katika Kijiji na Kata ya Mwaniko kilichiopo Wilayani Misungwi.

Amewataja waliouawa kuwa ni Nzuri Kazungu (25), mkazi Inchobela na Nkula Lameck (26), mkazi wa Mwamanga waliokuwa wamebeba Mpunga kwenye Pikipiki aina ya Kinglion yenye namba za usajiLi MC 989 CWU na kwamba wahusika walijichukulia sheria mkononi huku wakijua kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Kamanda Mutafungwa amesema, ”Pikipiki nayo ilichomwa moto na kuteketea kabisa wakati wa tukio hilo watu hao wakitokea kijiji cha Budula-Ngudu Wilayani Kwimba na walipofika Kijiji cha Mwaniko Wilayani Misungwi ndipo walipozuiliwa na kuuawa na wahalifu hao waliojichukulia sheria mkononi.”

Utawala Bora: Ujerumani yafurahishwa na kasi ya Rais Samia
Kibu Denis yupo Fit kuivaa Young Africans