Aliyekua meneja wa klabu ya Sunderland Gustavo Augusto “Gus” Poyet Domínguez, ameutaka uongozi wa klabu hiyo kumpa nafasi ya ajira Sam Allardyce.

Poyet, ametoa ushauri huo, kufuatia uongozi wa klabu hiyo kuendelea kuhangaika katika harakati za kumsaka mbadala wa Dick Advocaat ambaye alikubali kuondoka klabuini hapo mwishoni mwa juma lililopita kutokana na mambo kumuwa magumu kwake.

Poyet, amesema kuna ulazima kwa viongozi wa The Black Cat kutambua umuhimu na uzoefu wa Big Sam, ambaye kwa sasa hana kazi baada ya kuondoka Upton Park yalipo makao makuu ya klabu ya West Ham Utd mwishoni mwa msimu uliopita, kufuatia kushindwa kufikia malengo aliyokua amepangiwa na viongozi wake.

Amesema ni vigumu kwa sasa, kwa viongozi wa klabu ya Sunderland kumpata meneja ambaye atakua na uwezo mkubwa wa kufikisha azma ya kusaka mafanikio katika kipindi hiki ambapo ligi imeshaanza, na badala yake amewasisitiza kutuliza akili na kuangalia umuhimu wa watu wanaofahamu utamu na uchungu wa ligi ya nchinI England.

Poyet, anaamini Big San ni chaguo sahihi kwa klabu hiyo kwa sasa, kutokana na kuwa na sifa zote za kuokoa jahazi ambalo limeonyesha kukosa nahodha mzuri mwanzoni mwa msimu huu.

Kama itakumbukwa vyema Poyet aliondolewa, Stadium Of Lights, miezi miwili kabla ya msimu wa 2014-15, haijafikia kikomo mwezi May kutokana na matokeo mabaya kumuandama, na ndipo alipoajiriwa Dick Advocaat, ambapo alifanikiwa kukinusuru kikosi cha klabu ya Sunderland kutoshuka daraja.

Lakini pamoja na mazuri hayo meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, alitangaza kuondoka Stadium Of Lights mwishoni mwa msimu, lakini majuma kadhaa baadae alirejea na kuendelea na kazi kabla ya kujiondoa tena mwishoni mwa juma lililopita kutokana na mambo kuwa mabaya.

FIFA Yabariki Adhabu Ya Siku 90
Chile Hatarini Kuwakosa Vidal, Sanchez