Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameitaka dunia kusitisha vita baridi kati ya Marekani na China na kusimamisha mizozo ili iweze kujikita katika mapambano dhidi ya COVID-19.

Guterres amesema dunia inachukua mwelekeo wa hatari na kuonya kuwa haiwezi kuhimili mustakabali ambapo mataifa mawili yanayoongoza kiuchumi yanaigawanya dunia.

 Katibu mkuu huyo amesema kinachohitajika sio serikali ya dunia, bali mazingira mazuri ya uongozi.

Marekani na China zipo kwenye vita baridi ya kiuchumi, kila nchi ikitengeneza sheria na sera zinazoweka mazingira magumu ya kibiashara kwa nchi nyingine.

Guterres ameendesha kampeni ya kumaliza mizozo yote ya kivita duniani ili kupambana na janga la virusi vya corona. Ameitaja baadhi ya mifano ya mafanikio katika juhudi hizo, ikiwemo usitishwaji wa mapigano nchini Cameroon na Colombia.

.

Suarez haishiwi vituko, afanya jambo Italia
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 23, 2020