Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema kuwa ni mpango wa Mungu kumshusha chini Mtume Mwamposa ili mizizi ya huduma izidi kuimarika zaidi.
Amesema kuwa tukio lililotokea na kupelekea vifo vya watu 20 katika kongamano ngamamno la mtume Mwamposa mjini moshi ni fundisho kubwa kwa wale watu waliokuwa wanahoji kwanini yeye anakuwa na walinzi wengi wakati wa ibada zake.
“Tukio hilo ni kama ajali zingine zote, tukio lile lilikosa tu utaratibu mzuri wa namna ya kukanyaga yale mafuta, mimi nikikutana naye nitamuambia kuwa Mungu anataka kumuinua na hii ni sauti ya Mungu, na watu wengi walikuwa wananilaumu kwanini na kuwa na walinzi wengi ni kwa sababu ya matukio kama hayo, na hili tukio linaonesha kuwa sisi tuko mbele ya wakati” amesema Gwajima.
Mara baada ya watu takribani 20 kupoteza maisha katika zoezi la kugombea kukanyaga mafuta ya upako, Jeshi la Polisi lilimshikilia Mtume Mwamposa kwa mahojiano zaidi na baadaye aliachiwa kwa dhamana.