Askofu wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima amesema kuwa ameomba radhi kwa wananchi wa DRC Congo baada ya kutoa kauli kuwa nchi hiyo imekubali kufanyiwa majaribio ya chanjo ya Covid 19.
Gwajima alitoa mahubiri ya kukemea kitendo hicho siku chache tu baada ya umoja wa madaktari kutoka nchini Ufaransa kusema kuwa itaanza kufanya majaribio ya chanjo za Corona
Akizungumza kwenye kipindi cha 360 cha kituo cha televisheni cha Clouds tv jijini Dar es salaam leo, Gwajima amesema alipewa taarifa zisizo sahihi kabla ya mahubiri yake
“Niliwaomba msamaha wakongo maana kabla ya ibada niliambiwa kuwa Kongo wameshaanza majaribio nikasema kwenye ibada lakini baadaye nikajua ukweli kwamba hakuna majaribio yoyote yale nikapiga simu kwa wakongo,”amsema Gwajima.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema Afrika sio sehemu ambayo chanjo ya corona itafanyiwa majaribio.