Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima amekemea tabia ya watumishi wa sekta ya Afya kudanganya na kuwataka kuwa na weledi katika utumishi wao ili kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt. Gwajima amesema hayo wakati alipofanya ziara katika Hospitali ya Wilaya ya Nansio Ukerewe Mkoani Mwanza na kubaini kuwepo malalamiko ya uhaba wa dawa kutoka kwa wananchi, yaliyowasilishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Cornel Magembe.
Katika hali ambayo hakutarajia Dkt. Gwajima ameelezea kushangazwa baada ya kusikia wagonjwa hawapewi Paracetamol licha ya kuwa alivyotembelea stoo alikuta dawa hizo zipo.
Aidha, Dkt. Gwajima ameshangazwa na namna mnyororo wa dawa unavyoendeshwa katika Hospitali hiyo, kwani inaonekana kuna uzembe na ubadhirifu mkubwa wa dawa ambao husababisha hasara kubwa kwa Serikali.