Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kutoa hukumu siku ya leo katika kesi inayomkabili Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ya kushindwa kuhifadhi silaha na risasi ambayo anaimiliki kihalali kutoka na sababu za kuumwa alizozitoa Mahakamani hapo Wakili wake Peter Kibatala.
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Godfrey Mwambapa ameiharisha kesi hiyo mpaka Agosti 30 mwaka huu ambapo shauri hilo litatolewa hukumu yake tena.
Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43) na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31).
-
Mabawa aja na kampeni ”Magufuli Baki” nchi nzima
-
Tanzania yaombwa msaada na Uturuki
-
Majaliwa: Serikali imedhamiria kumaliza tatizo la maji nchini
Inadaiwa kuwa, Machi 29 mwaka 2015, katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni A, washitakiwa walikutwa wakimiliki bastola aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 bila kuwa na kibali kutoka mamlaka inayohusika na silaha na milipuko.