Kama ilivyo kawaida ya mtumishi wa Mungu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima kutumbua majipu kwa namna yake, jana katika ibada amefunguka na kuweka wazi kuwa yupo mbioni kuwatumbua watu wasiojulikana waliohusika katikia shambulio la risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu.
Hivyo ameomba apewe muda wa siku chache kutumia mitambo yake ya chini kwa chini kuwasaka watuhumiwa hao.
”Nilikuwa nje ya nchi kwa zaidi ya siku 80, hivyo ‘network’ yangu ilikuwa chini, ssa nimerudi na kesho (leo) ninakwenda kuona Lissu mjini Nairobi, nikirudi nitawaeleza maendeleo yake kwenye ibada ya jumatano,” amesema Gwajima.
-
Mbowe aeleza mapya ya hali ya Lissu, Dereva wake naye alazwa
-
Familia yasusa mazishi ya mteka watoto Arusha
Aidha Askofu Gwajima leo amekwenda jijini Nairobi kumjulia hali Lissu, na ameahidi kulisaidia jeshi la polisi kuwabaini majangili hao waliohusika katika shambulio hilo.
”Nikirudi nitawaeleza maendeleo yake kwenye ibada ya jumatano,” amesema Gwajima.
Gwajima ametumia nafasi hiyo kuwapongeza madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma waliomtibu Lissu kabla ya kusafirisjhwa kwenda Kenya pamoja na viongozi wa kisiasa kutoka vyama mbalimbali waliofika hospitalini hapo kumjulia hali.
Hivyo amewaasa viongozi wa serikalini kuendelea kushirikiana katika hili na kusema kuwa mtu akipata matatizo uadui unapaswa kuwekwa pembeni kuungana na kuwa kitu kimoja ili kusaidiana katika kutatua matatizo hayo.