Wasemavyo waswahili kupitia msemo unaoishi karne na karne ‘Mafahari Wawili Katu Hawakai Zizi Moja’, lakini wakati mwingine msemo huu unaonekana kukosa nguvu kufuatia uelewa na utayari wa mwanaadamu aliojaaliwa na mwenyezi mungu.

Mwanaadamu amejaaliwa kusamehe na kusahau matukio yaliyowahi kumuumiza hata zaidi ya mara moja, jambo ambalo linaendelea kudhihirisha sifa na uwezo wa muumba wake.

Kwa kipindi kirefu aliyekua mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alikua hapiki chungu kimoja na Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima, lakini hali imekua tofauti kwa wawili hao baada ya kuonekana wapo pamoja.

Gwajima anaewania nafasi ya ubunge Jimbo la Kawe Dar es salaam kwa tiketi ya CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM), hii leo ameokana akiwa pamoja na Paul Makonda walipofika nyumbani Kardinali Polycarp Pengo.

Tukio hilo pia limedhihirisha kuisha kwa tofauti zilizokuwepo kati ya Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima Josephat Gwajima na Kardinali Polycarp Pengo ambaye aliwahi kumtolea maneno makali miaka kadhaa iliyopita, alipokua akiendesha ibada kwenye kanisa lake la ufufuo na Uzima.

Huu ndio utu na ubinaadamu ambao tunahimizwa kila siku za maisha yetu, kwani hatuijui kesho yetu.

Hongereni viongozi wetu kwa hili mlilotuonyesha nasi twapaswa kuiga mfano huu mzuri ili kujenga umoja, amani na mshikano kwa maslahi ya taifa letu hususan katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.

MUNGU IBARIKI TZ, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

Kigogo MSD ,na wenzie waendelea kusota rumande
Kasi ya magonjwa ya mlipuko yapungua-NEMC