Mbunge wa Kawe kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Josephat Gwajima, kwa mara ya kwanza leo Bungeni kazungumza, ambapo amemshukuru Rais Magufuli kwa kumrahisishia kuingia Bungeni, ambapo amesema Rais Magufuli ndiye alikuwa tofali katika ushindi wao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 13, 2020, Bungeni Dodoma, mara baada ya Rais Magufuli kumaliza kulihutubia Bunge hilo na Taifa kwa ujumla.

“Ukiwa unasafiri halafu ukawa unasimama kila mahali kumtupia mawe kila Mbwa anayebweka, hutofika safari yako,  Mh. Rais wacha Mbwa wabweke tuendelee na safari yetu ya kutimiza ilani ya kurasa 303, waache wabweke kwa raha zao wewe kaza mwendo”, amesema Mbunge Gwajima.

“Sisi wabunge tulioingia Bungeni kwa mara ya kwanza ‘performance’ yako ya miaka mitano iliyopita imetubeba sisi kwenye majimbo yetu na bila shaka tumepata kura kupitia wewe, ulikuwa ndiyo tofali katika ushindi wetu, kuna sehemu hatukuhitaji kupiga kura tulitaja jina lako tu”.amesema Gwajima

Waziri Mkuu apewa jukumu hili la kwanza
Rais Magufuli afungua rasmi Bunge la 12