Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, amezitaka Bodi na Mabaraza yote ya kitaaluma ya sekta ya afya kujipanga kurejesha asilimia ya fedha wanazokusanya kwenye Mikoa na Halmashauri
Ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Bodi Mpya ya Ushauri wa Hospitali Binafsi iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma
Gwajima amesema fedha hizo zitasaidia wasajili wasaidizi kuwajibika katika ngazi za mikoa na halmashauri na kuharakisha zinawahudumia wananchi.
Naye Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya ushauri wa hospitali binafsi ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Aifelo Sichalwe amesema kuwa Serikali ya awamu ya sita inatambua mchango wa sekta binafsi hivyo itaendelea kutoa mashirikiano kwenye eneo hilo pamoja na yale ya nchi nyingine .
Uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali binafsi ni moja ya maswala yanayoashiria utekelezaji wa ilani ya uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020-2025 kwa upande wa sekta ya afya kwa kuwa Serikali itaimarisha na kuhakikisha jamii inapata huduma za afya zilizo bora na salama kwa ushirikiano na Sekta binafsi.