Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorothy Gwajima amewataka wanawake kuwa vinara kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto nchini.
Dkt. Gwajima amesema elimu zaidi kwa kutumia wataalam wa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii itumike kubadilishabfikra za jamii ili iweze kushiriki kataka kupambana na vitendo vya ukatili hasa kwa jamii kujikita kunako mapambano hayo hasa kuchangia rasilimali fedha na nguvu kazi ili kuondokana na vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa Wanawake wanatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwalinda Watoto na vitendo vya ukatili hasa unaotokea nyumbani na shuleni kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika Malezi na makuzi kwa mtoto
“Wanawake tuwe mstari wa mbele katika kupambana na vitendo vya ukatili ila hasa katika kujikwamua kiuchumi kwa kujishughulisha katika shughuli za maendeleo ili kupunguza vitendo hivyo ambavyo sababu kubwa ni uchumi,” alisema Waziri Dkt. Gwajima
Aidha ameiasa jamii kutimiza wajibu wao kwa kutofumbia vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na Makundi kwa kutoa taarifa na kuwa mstari wabele kutoa elimu kwa jamii kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanikisha azama hiyo ili kuwa na kizazi kilicho salama.
Naye, Naibu Waziri Mwanaidi Ali Khamis amesema kuwa Wizara inaungana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inashirikiana na kutoa elimu kwa jamii kuhusu madhara ya ukatili katika jamii na kuwaalika wadau wengine kujitokeza kuonganisha nguvu pamoja na Serikali katika mapambano hayo.
“karibu wadau mbalimbali katika Wizara yetu tushauriane na kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha tunaikomboa Jamii dhidi ya vitendo vya ukatili unaendekea kutokea kila kukicha nchini,” alisema Naibu Waziri Mwanaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Zainab Chaula ameswashukuru Wanawake vinara na kuwahakikishia ushirikiano kwenye kuhakikisha nguvu kubwa inawekwa kutoa elimu kwa jamii ili iondokane na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya Wanawake na Watoto.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum inaendelea kukutana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha inaweka mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.