Mshambuliaji Thomas Muller ametangaza kuastaafu kuitimikia Timu ya Taifa ya Ujerumani, saa chache baada ya kushindwa kuisaidia timu hiyo kutinga hatua ya 16 Bora, katika Fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Qatar.
Ujerumani ilishindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza Hatua ya 16 Bora, licha ya ushindi wa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Costa Rica katika mchezo wa mwisho wa ‘Kundi E’ jana Alhamis (Desemba Mosi).
Muller amesema mchezo huo ulikua wa mwisho kwake kuitumikia Timu ya Taifa ya Ujerumani, hivyo hana budi kumshukuru kila mmoja ambaye alifanikisha safari yake ya kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa FC Bayern Munich amesema alijitahidi kadri ya uwezo wake kwa kushirikiana na wengine, Ujerumani ifanikiwe kusonga mbele katika FAinali za Kombe la Dunia za mwaka huu, lakini hawakufanikiwa.
“Ulikuwa mchezo wangu wa mwisho kuitumikia timu ya Ujerumani, katika kipindi chote nilichokua katika timu hii nimeishi kwa furaha kubwa,”
“Asante kwa kila mmoja aliyefanikisha safari yangu ya kuitumikia timu hii. Siku zote nilijaribu kuonyesha moyo wa kupambana uwanjani, kuna wakati fulani kulikuwa na machozi ya furaha, wakati mwingine maumivu.” amesema Müller
Thomas Müller alianza kuitumikia Timu ya Taifa ya wakubwa ya Ujerumani mwaka 2010, akicheza michezo 121 na kufunga mabao 44.
Mshambuliaji huyo amecheza Fainali nne mfululizo za Kombe la Dunia akianzia Afrika Kusini (2010), Brazil (2014), Urusi (2018) na Qatar (2022).