Uongozi wa Ihefu FC uko kwenye mazungumzo ya kumpata aliyekuwa beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ baada ya mkataba wake na timu hiyo ya Manungu mkoani Morogoro kufikia kikomo.

Ihefu FC inatumia nafasi hiyo kumpata nyota huyo baada ya kuondokewa na Yahya Mbegu aliyejiunga na Singida Fountain Gate.

Taarifa ambazo zimepatikana kutoka ndani ya viongozi wa Ihefu FC zinaeleza makubaliano kati yao na mchezaji yamekamilika na kilichobaki ni kumwaga wino muda wowote ili kuichezea timu hiyo.

“Kutakuwa na mabadiliko makubwa ya kikosi chetu msimu ujao kwa sababu ya mashindano mbalimbali lakini suala la nani anaingia tutaliweka wazi tutakapokamilisha taratibu zote,” kimesema chanzo hicho.

Akizungumzia hilo Katibu Mkuu wa Ihefu, Zagalo Chalamila amesema hawezi kuzungumzia suala la beki huyo kwa sasa kwani bado wanaendelea na mazungumzo ya kupata nyota wakali watakaowaongezea nguvu.

Baba Ubaya anakuwa ni mchezaji wa pili kutoka Mtibwa na kutua Ihefu msimu huu baada ya kuondoka kwa, Charles Ilanfya.

Nyota mwingine aliyetua Ihefu FC ni mshambuliaji Meameroon, Moubarack Amza aliyeachana na Coastal Union ya Tanga.

Ally Kamwe: Kuna kazi nzito 2023/24
Mmoja akamilisha usajili Geita Gold FC