Mshambuliaji kinda wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland ameweka wazi kuwa beki wa kati kutoka nchini Senegal na klabu ya SSC Napoli ya Italia Kalidou Koulibaly, ni moja kati ya mabeki bora zaidi duniani.

Haaland amesema, beki huyo ana sifa za kipekee na amekua na umakini mkubwa wa kuwakaba washambuliaji hasa wenye makali, hivyo hana budi kuweka hadharani kwa kusema Koulibaly ni beki bora.

Mshambuliaji huyu alimtaja Koulibaly alipohojiwa na chombo cha habari cha Norway, ambacho kilimuhoji kuhusu changamoto alizowahi kukutana nazo uwanajani, na ndipo alipomtaja Koulibaly.

Wengine waliotajwa na Haaland kama mabeki bora duniani ni beki wa klabu bingwa nchini Hispania Real Madrid Sergio Ramos pamoja na beki wa mabingwa wa England Liverpool Virgil van Dijk.

“Nathani walinzi bora watatu duniani ni Sergio Ramos, Virgil van Dijk na Kalidou Koulibaly. Hawa wote watatu ni wana miili, lakini pia wana akili sana kwa namna wanavyocheza” amesema Erling Haaland

Halaand alikutana na karaha za Kalidou Koulibaly wakati wa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu wa 2018/19, wakati wa akiwa na klabu ya FC Salzburg.

Ubora wa Kolibaly ulifikia hatua ya kuzigonganisha klabu za Liverpool, Manchester City, PSG na Manchester United zilizokua na lengo la kumsajili, lakini uongozi wa SSC Napoli ulifanikiwa kubaksha beki huyo, kwa kumsainisha mkataba mpya.

Simba SC kuikaribisha Ihefu FC
Zlatan Ibrahimovic hadi 2021