Wananchi wa Vijiji vya Zepisa A na B vilivyopo kata ya Hombolo jijini Dodoma, wameiomba Serikali kuwapatia huduma ya maji, umeme na Barabara, ili kuwatoa kwenye kisiwa cha umasikini kutokana na kukosa huduma hizo muhimu licha ya nchi kuishi ndani ya Makao Makuu ya Nchi.
Wakizungumza kijijini hapo, baadhi ya Wananchi hao wamesema wamekuwa wakipata changamoto ya ukosefu wa maji kwa kipindi kirefu ubovu wa Barabara hususani kipindi cha Mvua na kutokuwa na umeme ndani ya Vijiji hivyo na kuathiri huduma kwenye kituo cha Afya.
Wamesema, “tunaiomba Serikali kutuletea huduma hizi ambazo ni muhimu sana, tunaishi ndani ya jiji ambalo ni makao makuu ya nchi lakini hatuna maji, umeme na barabara mbovu ambazo haziwezi kupitika kipindi cha mvua na kuhatarisha watu kukosa huduma.”
Hata hivyo, baadhi ya ya Viongozi walizungumzia changamoto zinazowakabili Wananchi wa Vijiji vya Zepisa A na Zepisa B wakisema, kero zinazolalamikiwa ni sahihi kwani zinawaathiri na wao.