Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Habibu Kondo amesema wamepanga kuchukua pointi tatu za kwanza msimu huu kwa kuwafunga Dodoma Jiji FC katika mchezo wa ligi Kuu Bara utakaopigwa keshokutwa Ijumaa (Septemba 15), Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Mtibwa inayoshika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ipikiwa na point moja haijaonja ladha ya ushindi katika mechi zake mbili za awali ilizocheza uwanja wake wa nyumbani, Manungu Complex, Morogoro.

Kocha huyo amesema mapumziko ya muda mrefu ya ligi yamemsaidia kurekebisha mapungufu ambayo aliyabaini kwenye mechi mbili walizocheza awali, hivyo wanakwenda kuivaa Dodoma Jiji wakiwa imara.

“Tumezitumia vizuri wiki mbili za mapumziko, makosa yaliyosababisha tukashindwa kupata ushindi nyumbani tumeyarekebisha na tupo tayari kuanza ligi tukiwa ugenini kwa kuifunga Dodoma Jiji ingawa mchezo utakuwa mgumu” amesema Kondo.

Kondo amesema katika mechi mbili zilizopita makosa yao yalikuwa kwenye safu ya ulinzi na usambuliaj, wameyarekebisha na mechi za karafiki walizocheza zimewasaidia kubaini kuwa wapo tayari kwa ushindani. Timu hiyo lipoteza mechi yake ya kwanza ikifungwa mabao 4-2 na Simba SC kabla ya kutoa sare ya 1-1 dhidi ya Coastal Uion ya Tanga.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 14, 2023
Phiri, Chama waachiwa kazi Zambia