Baada ya hivi karibuni Lionel Messi kukubali kusaini mkataba wa kuendelea kusalia Camp Nou kwa miaka mitano licha ya kupunguzwa asilimia 50 ya mshahara wake (kutoka Bili 2.7 hadi Bil 1.3 Tzs) kwa wiki, huko Italia nako Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuendelea kubaki Turin kwa kukatwa mshahara pia.
Kabla ya taarifa hii kulikuwa na ripoti kwamba staa huyo huenda akaondoka Juve katika dirisha hili ambapo miamba hiyo ya Italia ilikuwa inataka kumuachia ili kupunguza matumizi katika timu kutokana na mshahara wake wa Euro 900,000 (Bilion 2.4 tzs) anaopokea kwa wiki.
Lakini taarifa za kuaminika kutoka Juventus zinadai Mazungumzo baina ya wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes na mwenyekiti wa Juve, Andrea Agnelli yameanza na suala la kumkata mshahara linatarajiwa kukamilika kabla hajarudi kuungana na Juve kwenye mazoezi ya maandalizi ya msimu ujao
Kwa sasa Ronaldo anakula bata na mchumbawake Georgina Rodriguez kwenye boti yao ya kifahari yenye thamani ya Pauni milioni 5.5.