Beki wa kushoto wa kikosi cha Dar es salaam Young Africans, Haji Mwinyi amesema kuwa alitumia mapungufu aliyoyaona kwa Oscar Joshua ambayo yalimpa nafasi ya kuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha Hans Pluijm.

Mwinyi alisema kuwa mbinu pekee aliyoutumia kupata nafasi kwenye kikosi hicho ni kusikiliza kwa umakini maelekezo aliyokuwa akiyatoa kocha wao kwa Joshua na Edward Charles na kwenda kuyafanyia kazi nje ya kikosi hicho.

Mazoezi pekee aliyokuwa akiyafuatilia ni jinsi ya kumiliki mipira na stamina ambayo aliyawekea mkazo hatimaye alifanikiwa kumpokonya namba Joshua.

“Kiukweli nilikuwa nasikiliza sana maelekezo yaliyokuwa yanatolewa kwa Joshua na Edward bila wao kujua na mimi nilikuwa naenda kuyafanyia kazi kivyangu, nikija mazoezini naonyesha uwezo wa kumiliki mipira na hatimaye kocha akanikubali na kunipa nafasi.

“Nafahamu kuwa Joshua ni mchezaji mzuri na mzoefu hivyo siwezi kubweteka kwani safari yangu bado ni ndefu mno hivyo natakiwa kujituma zaidi kwani kupata namba ndani ya kikosi cha Yanga ni kazi kubwa sana,” alisema Mwinyi

Mayanga: Haikuwa Rahisi Kuwafunga Toto Africans Kwao
Ufisadi wa Miss Tanzania wapelekea Serikali Kuishushia rungu zito benki ya Stanbic