Majane wa Rais aliyeuawa Haiti, Jovenel Moise amerudi nyumbani baada ya kutibiwa majeraha aliyoyapata katika shambulio lililochukua uhai wa Rais wa Nchi hiyo Julai 7.
Martine alilazwa katika hospitali ya Miami huko Florida nchini Marekani kwa siku 10 baada ya kushambuliwa pamoja na mumewe nyumbani kwao .
Waziri wa mawasiliano wa serikali Frantz Exantus kupitia mtandao wa twitter ameandika kwamba Martine Moise, alipokelewa katika uwanja wa ndege wa Port-au-Prince na waziri mkuu wa mpito Claude Joseph.
Mazishi ya kiongozi huyo yanatarajiwa kufanyika tarehe 23 huko Cap-Haitien, jiji la kihist