Msemaji wa klabu ya Young Africans Haji Manara amechekelea kichapo cha 2-0 walichokipokea Simba SC kutoka kwa RS Berkane ya Morocco jana Jumapili (Februari 27), katika michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Simba SC ilikua na kazi nzito ya kupambana katika mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa Kundi D, kwenye michuano hiyo ukiwa mchezo wake wa pili mfululizo kucheza nje ya Dar es salaam baada ya kuifunga ASEC Mimosas Kwa Mkapa mabao 3-1 mapema mwezi huu Februari.
Manara amechekelea kadhia hiyo iliyowakuta Simba SC ugenini, kwa kuandika maneno ya kebehi kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Manara ameandika: Team Banchikicha msisahau kupitia Ukraine kutuletea Chapati za Dengu,na Mishkaki ya Tumbili
Halaf hii ya kupokewa na Maua ndio imewatia nuksi kabisa, yaani huo ndio Ubanchikicha wenyew sasa Yaan Club ya Mpira ipokewe na Asumini au Maua ya Rose?
Ndio maana mlipakatwa kibwege bila Short on Target hata moja,,,,,muhimu msisahau kupitia ?? mtanikuta hapa.
Kichapo cha 2-0 kimeifanya Simba SC kuporomoka kutoka kileleni mwa msimamo wa Kundi D hadi nafasi ya pili kwa kuendelea kuwa na alama 04, huku nafasi ya kwanza ikishikwa na RS Berkane yenye alama 06 na USGN ipo nafasi ya tatu kwa kufikisha alama 04.
ASEC Mimosas iliyopoteza mchezo dhidi ya USGN kwa kukubali kufungwa 2-0, inaburuza mkia wa kundi hilo kwa kuendelea kuwa na alama 03.