Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara ameipiga kijembe Simba SC, kwa kugusia safari yao wa nchini Morocco kupitia Uturuki ambako walikaa kwa siku moja kabla ya kuendelea na safari.
Simba SC ilipitia Uturuki kufutia kusafiri na shirika la ndege la nchi hiyo alipokua wakitoka nchini Niger, hivyo walisubiri mjini Instanbul kwa ajili ya kuunganisha ndege iliyokua inaelekea nchini Morocco.
Marana amerusha kijembe hicho, baada ya Mashabiki na Wanachama wa Simba SC kutamba kuwa kikosi chao kilipitia Barani Ulaya (Uturuki) kwa ajili ya kubarizi kabla ya kuendelea na safari ya Morocco.
Muajiriwa huyo wa zamani wa Simba SC amesema, anashangazwa kuona Mashabiki na Wanachama wa Simba wakitamba kuhusu timu yao kufika Uturuki, ili hali Young Africans waliwahi kufanya hivyo miaka ya nyuma.
“Ni ajabu kusifia timu yao kufika Uturuki, Young Africans walifika huko zamani sana, tafuta kingine cha kuzungumzia” amesema Haji Manara alipokua akijibu swali la Mwandishi wa Habari aliyemuuliza kuhusu tambo na Mashabiki na Wanachama wa Simba SC.
Simba SC iliondoka Uturuki Jumatano (Februari 23) kuelekea Morocco, tayari kwa mchezo wa Mzunguuko wa tatu wa ‘Kundi D’ Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya RS Berkane.
Ikiwa Morocco Simba SC iliweka kambi kwa muda mjini Casablanca kabla ya kuifuata RS Berkane jana mjini Berkane, kwa ajili ya mpambano wa kesho Jumapili (Februari 27), utakaounguruma majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.