Mkuu wa kitengo cha idara ya habari na mawasiliano ya mabingwa wa soka Tanzania Bara (Simba SC) Haji Sunday Manara, amewajibu baadhi ya wadau wa michezo waliopokea tofauti kauli yake aliyoitoa mara baada ya Rais Magufuli kusisitiza mpango wa kuendelea kwa msimu wa ligi kuu msimu huu 2019/20.

Manara alitoa kauli na kusambaza taarifa za kumshukuru Rais Magufuli kwa kuendelea kutoa msisitizo huo, na Dar24 ilikua sehemu ya walioandika habari za pongezi zilizotolewa na mkuu huyo wa habari na mawasiliano wa Simba SC.

Katika Kauli/Taarifa yake Manara aliahidi kuwasilisha pendekezo kwa viongozi wa Simba SC, kukabidhi kombe la ubingwa kwa Rais Magufuli endapo watafanikiwa kutimiza azma ya kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo.

“Kwa kuwa Mh. Rais ndiye aliyeagiza ligi irudi hatuna ubaya wala si dhambi ukizingatia kombe hili la tatu mfurulizo, maanake ni letu yaani “TFF” hawatapata kombe tena ni mali yetu, tutampelekea hata Mh. Rais ikimpendeza akae nalo ikibidi likae ikulu na akaona vipi likae Magogoni si mbaya wala si dhambi, kombe hili ni la Simba na Simba tumelichukua moja kwa moja kumpa tunu ile Raisi wetu tutapungukiwa nini sisi.”

Mapema hii leo Haji ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram ujumbe ambao ni dhahir umewalenga walibeza shukurani zake kwa Rais Magufuli.

Manara ameandika: “Nikipost mambo ya Simba mnasema najiona kama Simba mali yangu na Yanga nao wanasema nawacharura sana,”

“Nikimpost @diamondplatnumz mnasema mimi ni team Wasafi, siku moja nilimpost @officialalikiba mkasema acha kujipendekeza, nikimpost Rais wa nchi au Wanachama wenzangu wa CCM mnasema natafuta cheo Serikalini, ipo siku nilim-wish birthday @professorjaytz wanaccm wakanilaumu kama nimeua vile!!”

“Nikipost nacheza Mziki napigiwa Astaghfirullah utadhani nimechoma moto Msikiti, nikipost habari za dini yangu wapo pia wanasema mm mbaguzi wa dini na siwapendi watu wa Imani nyingine, nikiwapost viongozi wa Dini nyingine naitwa kafiri mla Nguruwe, siijui kheri ya mja ni ipi !, hususan mja wa mitandaoni.” Ameandika Manara.

Mwisho Manara akaamua kumalizia na ujumbe ambao ameuelekeza kwa watu wanaombeza na kumpinga kila anapotoa kauli ama andiko kuhusu maono yake katika maendeleo ya sekta yoyote nchini.

“Sasa niwaambie hivi, Kwa wale wanaonipangia kitu cha kupost nitumieni picha za mama zenu au Shangazi zenu DM ili niwe nawapost wao mpate kufurahi, unless otherwise niacheni mwenyewe, ntaweka ntakacho mm, ukiona vp left in peace katika page hii, Haji nnaemjua mm hawezi kupangiwa nn apost au asipost tena katika page yake mwenyewe, Gastadialo!!”

Waziri Mkuu Lesotho ajiuzulu, tuhuma za mauaji ya mkewe
Mbowe na wenzake wanavyopambana kukwepa jela miezi 60

Comments

comments