Klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia inaripotiwa kuwa na shaka juu ya uhamisho wa Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Morocco Hakim Ziyech kutoka Chelsea, kwa mujibu wa Mail Sport.
Mchezaji huyo ni mmoja wa wachezaji kadhaa ambao wanawaniwa na Klabu za Saudi Arabia wakati wanaendelea na harakati zao za kusajili wachezaji kutoka Ulaya.
Chelsea hadi sasa imeshuhudia Edouard Mendy akikamilisha uhamisho wa kwenda Al-Ahli, Kalidou Koulibaly kwenda Al-Hilal, na N’Golo Kante kuondoka kama mchezaji huru na kujiunga na Al-Ittihad, huku Ziyech na Pierre-Emerick Aubameyang nao wakitajwa kuwa njiani.
Mahusiano mazuri ya The Blues hao na wajumbe kutoka kwa Klabu nne zinazomilikiwa na Mfuko wa Uwekezaji wa Umma wa Saudia yalivutia uchunguzi fulani kutokana na uwekezaji wa hazina ya utajiri katika Clearlake Capital.
Ziyech amekuwa na shida kwa dakika wakati wa msimu uliopita pale Chelsea, licha ya kuonesha kiwango cha kuvutia akiwa na Morocco kwenye Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.
Mchezaji huyo mzaliwa wa Uholanzi anaaminika kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu wa klabu hiyo uliobaini matatizo ya goti jambo ambalo limezua wasiwasi kuhusu kuhamia kwenye timu hiyo ambayo yupo Cristiano Ronaldo.
Tatizo kama hilo hapo awali lilitambuliwa na Paris Saint-Germain wakati wa kumnunua mchezaji huyo kwa mkopo wakati wa dirisha la Januari.
Uhamisho huo hatimaye haukufaulu kutokana na suala la kiutawala muda mfupi kabla ya tarehe ya mwisho kwa upande wa Chelsea, ambayo ilizidisha kufadhaika kwa Ziyech wakati msimu unamalizika. Katika mashindano yote, Ziyech alifunga mabao 14 na kusajili asisti 13.