Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuharibu amani na usalama tuliojenga kwenye Taifa la Tanzania.

Dkt. Samia ameyasema hayo katika Maadhimisho ya Miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Chuo cha Tumaini Makumira Mkoani Arusha, hii leo Agosti 21, 2023.

Amesema, “ndugu zangu na haswa baba Askofu Shoo, kaka yangu Askofu Mkuu wa kanisa. Nimeyasikia yote uliyosema kuhusu usalama, amani, umoja na mwendelezo wa Taifa letu. Niliamua kunyamaza kimya na naendelea kunyamaza kimya.

Aidha, Rais Samia ameongeza kuwa, “ninachotaka kuwahakikishia, hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuligawa Taifa hili. Hakuna mwenye misuli na ubavu wa kuuza Taifa hili.”

Zimbabwe wafanya ibada kuombea uchaguzi Mkuu
Wanawake CHADEMA wafundwa fursa kiuchumi, matumizi ya Fedha