Baada ya kusambaa kwa picha katika mitandao ya kijamii na uvumumi kwamba msanii wa bongo fleva Dogo janja amemuoa muigizaji wa filamu Irene Uwoya sasa ukweli umefahamika.

Inaonekana kuwa hakuna ndoa kati ya Dogo janja na Irene Uwoya, hii imekuja baada ya msanii Keisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kupost picha ya pamoja akiwa na Babutale, Madee, Kasim Mganga, Irene Uwoya na Dogo janja na kuandika ”Ahsanteni sana familia yangu kwa ushirikiano wenu the real queen of bongoflava is back the video is cumin soon”.

Keisha ametegua kitendawili baada ya ujumbe huo kwenye Instagram na ukweli ni kwamba kuna video ya muziki ya wimbo wa Keisha inayotarajia kutoka hivi karibuni ambayo imewashiriksha Dogo janja na Irene Uwoya wakiwa kama wanafunga ndoa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Zitto Kabwe akamatwa na jeshi la Polisi
Ndugai: Tatizo wana washwa washwa