Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka Wananchi kupuuza taarifa kuwa katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwezi AgostI mwaka huu kuna kipengele kinachohusu dini.
 
Amesema jambo hilo halipo na halijawahi kuwepo katika Sensa zote za Watu na Makazi ambazo zimewahi kufanyika nchini.
 
Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati akihutubia katika maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani kwa upande wa Zanzibar, ambapo yeye alikuwa ni mgeni rasmi.
 
 
Amesema kipengele kipya kilichoongezwa katika Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka huu ni anuani za Makazi na kuwataka Watanzania wote kutoa ushirikiano ili kufanikisha jambo hilo.
 
Kauli mbiu ya kitaifa ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka huu ni kizazi cha haki na usawa kwa maendeleo endelevu, jitokeze kuhesabiwa.

Mbowe aeleza sababu zilizomkutanisha na Rais Samia
Rais Mwinyi aahidi mazito kwa wanawake