Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela amesema endapo kila Mtanzania angekuwa akifanya kazi na kusimamia majukumu yake ipasavyo changamoto mbalimbali ikiwemo za uwepo wa watoto wa mtaani sizingekuwepo na kutaka kila mtanzania kuondoa changamoto zake mwenyewe.

Kasesela ameyasema hayo nyumbani kwake mjini Iringa wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media na kuongeza kuwa usimamiaji wa majukumu na uwajibikaji wenye kujali maisha ya watu wengine, husaidia kuondosha sintofafamu zilizopo kwenye jamii.

Amesema, “utakuta mtu ana mtoto au wazazi wana mtoto lakini hawamtaki na ukichunguza kwa makini huwezi pata majibu yenye mashiko, mzazi anamuacha mtoto ajihangaikie hampi uelekeo wa maisha, hampi elimu hapo unatarajia nini Kama si kuzalisha watoto wa mitaani.”

Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela.

Aidha, Kasesela ambaye ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi – CCM, NEC amesema kila mwanajamii anatakiwa kuishi maisha ya kujitoa kwa ajili ya wengine, kusimamia kila hatua za maisha yake na watoto ili kusaidia ukuaji wa Taifa lenye mwelekeo sahihi na kupunguza adha zilizopo katika jamii.

“Unapopata changamoto muathirika wa kwanza ni wewe, na maumivu au athari zinakukuta wewe mwenyewe, hii misaada au usaidizi unakuja baadaye na ukija basi ukutwe umepata ahueni vipi ukiwa haupo? kwahiyo ni muhimu kujipanga ili kukabiliana na changamoto za mbele yako, hakuna wa kukuondolea changamoto zako pambana nazo mwenyewe,” amefafanua Kasesela.

Robertinho afichua usajili Simba SC
Vita kupanda Ligi Kuu, viongozi wa mikoa watambiana