Waziri wa afya, Ummy Mwalimu amewataka watoa huduma za afya nchini kote kuacha tabia ya kuwatoza fedha wakinamama wajawazito pindi wanavyofika Kliniki kupata huduma.

Waziri Ummy ametoa kauli hiyo jijini Tanga mara baada ya kutembelea kituo cha afya cha Makorora na kujionea hali ya utoaji huduma.

“Naomba nisisitize hili si hapa tu bali ni nchi nzima,acheni tabia ya kuwatoza fedha kinamama wajawazito pindi wanapofika cliniki kupata huduma”amesema waziri Ummy

Aidha Waziri Ummy ameongeza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kuongeza kasi ya usambazaji wa dawa katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya hapa nchini.

TET yateta na maofisa wa REDEOA
Jeshi la Polisi kuja na ripoti ya mauaji