Mchezaji namba mbili kwa ubora katika mchezo wa tenesi nchini Romania Simona Halep ameweka historia yake kwa mara ya kwanza kwa kumshinda Maria Sharapova katika michuano ya China Open hatua ya robo fainali.

Halep mwenye umri wa miaka 26 alitumia muda wa dakika 73 kumshinda Maria Sharapova kwa seti 6-2 6-2 katika mchezo huo.

Sharapova alijikuta anashindwa kabisa kufurukuta Halep aliyecheza kwa kiwango cha juu na mwisho wa mchezo akasema Halep alikuwa mzuri kushinda yeye.

Halep kwa sasa atakutana na Daria Kasatkina wa Urusi ambaye alimchapa Agnieszka Radwanska kwa seti 4-6 7-5 6-2.

Mara ya mwisho kwa Sharapova kumshinda Halep ilikuwa katika michuano ya US Open mwezi Agosti.

Video: Gongo yaua watu 19 Dar, Siku 30 moto CCM, Ukawa
Gambo: Lema anapoteza muda wake bure