Mambo hayaendi vizuri kwa nyota wa Manchester United, Antony juu ya madai yake ya unyanyasaji wa kijinsia ambayo kwa sasa yamefikia wanawake watatu, huku yeye akifunguka kuwa huo ni mpango uliopangwa makusudi ili kumtoa kwenye njia.

Anthony, amekanusha madai yote ya unyanyasaji aliyoelekezwa na wanawake kadhaa alipofanya mahojiano na kituo kimoja cha TV (Fofocalizando), nchini kwao Brazil.

Mpenzi wa zamani wa Antony, Gabriela Cavallin hivi karibuni alijitokeza na kudai kuwa winga huyo wa Man United alimshambulia kinyanyasaji mara nne.

Baada ya hapo wanawake wengine wawili wamejitokeza na kutoa madai sawa, Rayssa de Freitas na Ingrid Lana.

Antony, alikanusha madai yote ya unyanyasaji na kusema haogopi mustakabali wake Old Trafford, ingawa anajua ni mpango wa kuharibu maisha yake ya soka.

Kwenye mahojiano alionekana akibubujikwa na machozi na kusema: “Ni jambo ambalo haliingii akilini, ukweli utajitokeza, najua kuna watu wengi wananichukia, lakini ukweli utadhihirika.”

Upande wa pili kuna taarifa kwamba baada ya tukio hilo United ilituma madaktari wa klabu kumhudumia Cavallin (Ex wa Antony) baada ya kusisitiza kuwa alikuwa amejeruhiwa vibaya. Antony mwenyewe anasema siku ya tukio.

“Nilitaka kumwambia nina majukumu na na lazima niende, hivyo alichukua sahani na vikombe na kuvitupa chini na mimi nikamshika ili kumtuliza sikumuumiza wala kumjerui kama anavyodai.”

Cavallin ameenda mbali na kusema moja ya vipandikizi vyake vya matiti vinahitaji kubadilishwa kutokana na unyanyasaji aliofanyiwa na Antony.

Wanafunzi wahimizwa kukataa ndoa za utotoni
Tetemeko Morocco: Idadi ya vifo yafikia Watu 2900