Maafisa wa Kremlin wameilaumu Ukraine kuhusika na shambulio la roketi lililoipiga ofisi ya meya katika mji muhimu wa Ukraine, unaodhibitiwa na wanaotaka kujitenga, wakati vita vya Urusi vikikaribia miezi minane.

Mashambulizi hayo, kwa pande zote yamefanyika wakati Urusi imeshindwa kushikilia maeneo iliyoyadhibiti katika muda wa karibu wiki saba tangu vikosi vya jeshi la Ukraine vilipoanza mashambulizi yake ya kusini.

Shambulio la roketi lililoipiga ofisi ya Meya katika mji wa Ukraine. Picha: WYFF

Wakati huohuo, maafisa wa Ukraine wamesema roketi za Urusi zilipiga mji wa upande mwingine kutokea kiwanda cha nyuklia za Zaporizhzhia, na kujeruhi watu sita.

Wiki iliyopita, katika hatua ya kulipa kisasi Urusi ilianzisha kile ilichoamini kuwa mashambulizi yake makubwa zaidi yalioratibiwa ya anga na makombora dhidi ya miundombinu muhimu ya Ukraine, tangu kuanza kwa uvamizi wake Februari 24.

Ruto avunja kitengo maalum cha Polisi
Wito mpya kuwekeza kwa vijana Afya, Biashara