Wakati mashabiki wa klabu bingwa Tanzania Bara Simba SC wakisubiri taarifa rasmi kuhusu hali ya beki wa pembeni Shomari Kapombe, inaelezwa kuwa hali ya beki huyo sio ya kutisha sana.
Beki huyo kipenzi inadaiwa alipata majeraha kidogo kwenye mguu wake pamoja na hasira alizokuwa nazo zilimfanya ashindwe kuwa kwenye ubora wake.
Kapombe alichezewa faulo na mchezaji wa Azam FC, Frank Domayo jana, Julai Mosi Uwanja wa Taifa wakati Simba SC ikishinda maba mawili kwa sifuri kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.
Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa baada ya kupewa huduma ya kwanza, Kapombe aliweza kusimama na kutembea mwenyewe jambo linalomaanisha kwamba hana majeraha makubwa.
“Ilikuwa ni hali ya mshtuko aliyoipata pamoja na hofu ya kutumia ukichanganya na hasira vilimfanya awe katika hali ile ila leo atafanyiwa vipimo kwani jana aliweza kusimama baada ya kupewa huduma ya kwanza a kupunguza hasira,” ilieleza taarifa hiyo.
Sven Vandenbroec, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa mpaka atakapochukuliwa vipimo ndipo watazungumzia hali yake.
Katika hatua nyingine Kiungo wa Azam FC Frank Domoyo ameendelea kumtaka radhi Shomari Kapombe kwa rafu mbaya aliyomchezea kwenye mchezo wa jana.
Domayo amesema haikua dhamira yake kufanya vile, na kilichotokea ni bahati mbaya, na anaendelea kujutia kosa hilo.
“Naomba radhi kwa kilichotokea. Haikuwa kusudi langu kumchezea rafu (Kapombe) bahati mbaya tempo ilikuwa juu”
“Nakuomba radhi nilimfuata kutaka kuongea naye akataka kunipiga nitampigia simu nimuombe radhi kikubwa anisamehe ukiwa kwenye mpira unakuwa na tempa kubwa Kama vile umefungaa, Hasira yote kwa yote naomba anisamehe”- Frank Domayo kuhusu kumuomba radhi Shomary Kapombe