Mbunge wa Kawe(Chadema), Halima Mdee anashikiliwa na jeshi la Polisi katika kituo kidogo Cha Oysterbay kwa amri ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ilyotolewa Jana.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na Chadema kupitia ukurasa wa Twitter, Mdee anashikiliwa baada ya kujisalimisha kituoni hapo ambapo alikwenda ili kumuona Mkuu wa upelelezi wa mkoa wa kipolisi Kinondoni (RCO).
Taarifa iliyotolewa na Polisi, Mdee atakaa chini ya kizuizi Hadi jumanne ijayo Novemba 19 ambapo atafikishwa mahakamani.
Ikumbukwe kuwa Jana Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ilitoa amri kuwa wabunge wanne wa Chadema wakamatwe kutokana na kuvunja masharti ya dhamana zao, miongoni mwao Ni Mdee.
Wabunge wengine ambao wanatakiwa kukamatwa Ni, Ester Bulaya, Mchungaji Peter Msigwa, na John Heche.