Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Mkoani Pwani imetenga kiasi cha sh. bil 5.3 kwa ajili ya ujenzi wa makao makuu ya wilaya hiyo.
Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Yusufu Mbinda wakati akizungumzia baadhi ya utekelezaji wa masuala ya miundombinu ya maji, chakula na mifugo.
Amesema kuwa wametenga mil. 969.1 zitakazotumika katika ujenzi wa daraja la Mwake lenye urefu wa mita 40 ili kurahisisha mawasailiano ya njia ya barabara .
Aidha, ameongeza kuwa wakandarasi wanafanya utafiti wa vyanzo vya uchimbaji visima katika vijiji mbalimbali lengo likiwa kuwaondolea kero ya ukosefu wa maji wananchi.
Hata hivyo, Mbinda amevitaja baadhi ya vijiji vinavyotarajia kunufaika na mpango huo kuwa ni Nyamisati, Mtunda, Mchungu, Mahege na Kivinja A.
-
Makonda kupitia upya taaluma za wanasheria, asimamisha kesi zote
-
Video: Makonda awatumbua wakuu wa Idara za Ardhi
-
Makonda nusura aue mtu Jijini Dar