Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa kuhakikisha wanakamilisha Ujenzi wa Shule ya Msingi Msagali ndani ya muda wa wiki mbili baada ya kutokamilika kwa muda uliopangwa awali Juni 30, 2023.

Senyamule ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mpwapwa kukagua miradi na miundombinu inayojengwa katika Shule hiyo Mpya ya Msagali inayojengwa kupitia fedha za Boost na Shule ya Sekondari Mazae kupitia fedha za Serikali Kuu.

Aidha, kiasi cha ya shilingi Milioni 493 zimetolewa kupitia mradi wa boost kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya viwili vya madarasa ya mfano kwa Elimu ya awali vyeye matundu sita ya vyoo, Vyumba 14 vya Madarasa, Matundu ya vyoo 16, Jengola Utawala, Kichomea taka, madawati, viti na meza katika Shule ya Msingi Mpya ya Msagali.
 
Pia, kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 730 zimetolewa katika Shule ya Sekondari Mazae kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa tisa, Mabweni manne na Matundu ya vyoo 14 huku akisema “nawapatia wiki mbili hii shule iwe imekamilika hakikisheni mnachukua hatua na kuandaa mpango kazi ambao utakamilisha kazi hii kwa haraka pia vifaa vyote vinunuliwe, hapa najua pamoja na yote mnayojitetea kuna chembe chembe ya uzembe.”

Bingwa CECAFA wasichana kupatikana Chamazi
Parimatch yaidhamini Geita Gold FC