Kampuni ya simu za mikononi Halotel imetoa msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano ya namba ya dharura 114, katika makabidhiano yaliyofanyika mchana wa leo Jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo ambayo ilifanyika Makao Makuu ya Halotel Naibu Mkurugenzi. Trieu Binh, amesema kuwa wametoa msaada huo ili kusaidia jamii kuwapata haraka Jeshi la Zimaoto na Uokoaji kwa kutumia matandao wa halotel.

Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Billy Mwakatage, amesema kiuwa msaada huo utakuwa ni chachu kwa Jeshi na utarahisisha mawasiliano kati ya Jeshi na jamii wakati yanapotokea majanga.

Aidha, ameahidi kuzigawa simu hizo kwenye vituo vya Zimamoto na Uokoaji hapa nchini ili kuongeza wigo mapana wa mawasiliano haswa kwa wateja wa halotel kwani mwanzo huduma hiyo ilikuwa haipatikani kwa kupiga 114.

Hata hivyo, Mwakatage ameishukuru Kampuni hiyo kwa msaada walioutoa na kuwaomba waendelee kushirikiana na Jeshi hilo katika nyanja nyingine mbalimbali ili kuboresha huduma kwa jamii.

Video: Makonda awataka Tanesco kuimarisha huduma ya umeme
Ligi kuu bara kuendelea wikiendi hii