Chama cha Alliance for Democratic Change ADC kimeadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwake huku kikiwataka wanasiasa nchini kuwa wakweli na kuendelea kudumisha amani badala ya kutoa kauli na ahadi ambazo zina mwonekano wa kutaka kuleta mpasuko.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Taifa wa ADC ambaye pia ni Waziri wa Kilimo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hamad Rashid Mohamed, alipokuwa kuwa katika maadhimisho ya miaka mitano ya chama hicho.
Amesema kuwa kauli tata zenye viashilia vya uchochezi hazikubariki kamwe kwani zinaweza kusababisha mpasuko katika jamii kitu ambacho kinaweza kusababisha madhara makubwa.
-
Mbowe aonya kuhusu kauli za viongoz
-
Lissu: Sijui wanaogopa kutumbuliwa
-
Zitto Kabwe: Hatukutaka mnunue ndege hovyo hovyo
Hata hivyo, Kwa upande wake Katibu Mkuu wa ADC, Doyo Hassan Doyo, amevitaka vyama vingine vya upinzani kujenga tabia ya maridhiano pamoja na kusameheana, kama njia ya kumaliza migogoro inayoendelea ndani ya vyama hivyo, kama ambavyo ADC imefanya hivi karibuni kwa kuwasamehe wanachama wake ambao walifukuzwa uanachama miaka michache iliyopita.