Gwiji wa soka wa Ujerumani Didi Hamann, amautahadharisha uongozi wa Bayern Munich, kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa Manchester City Leroy Sane.
Bayern Munich inatajwa kuwa kwenye mpango wa kumsajili mshambuliaji huyo mwishoni mwa msimu huu, kwa kuamini huenda wakampata kwa urahisi kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester City.
Hamann ameuambia uongozi wa mabingwa hao wa Ujerumani kuwa, wanapaswa kujikita kufikiria usajili wa mchezaji mwingine, na waachane kabisa na mpango wa kumsajili Sane.
Amesema ni bora kwa FC Bayern Munich wajipange kumsajili mshambuliaji Milot Rashica wa Werder Bremen.
Hamann amesema: “Ni vigumu kwa sasa kumfikiria mchezaji ambaye nidhamu yake haifahamiki, japo ana uraia wa Ujerumani, ameshaambukizwa tamaduni za Uingereza, na huenda ikamchukua muda mrefu kuzoea mazingira ya hapa Munich.”
Milot Rashica.
“Kila ligi ina mazingira na tamaduni zake, ni bora kumsajili mchezaji ambaye ana uzoefu mkubwa katika ligi ya hapa, naamini wakifanya hivyo watakua na nafasi kubwa ya kufurahia watakachokifanya mwishoni mwa msimu huu, lakini kwa Sane mimi siwashauri kabisa.”
“Klabu inahitaji mchezaji mwenye kaliba ya ushambuliaji wa pembeni hususana anaecheza hapa Ujeruani, kinachotakiwa ni utulivu na kuangalia matarajio ya sasa na ya baadae ya klabu kubwa kama Bayern Munich ambaye inahitaji mafanikio kila msimu.”
“Ninaamini Rashica atakua mchezaji sahihi kwa Bayern Munich, kutokana na mwenendo wake kuwa mzuri kwenye ligi ya hapa.”
Rashica rais wa Kosovo, tayari ameshaitumikia Weder Bremen katika michezo 51 na kufunga mabao 17 tangu mwaka 2018 aliposajiliwa akitokea SBV Vetesse ya Uholanzi.