Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa Silaha haramu wa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna Msaidizi wa Polisi, Berthaneema Mlayi amewataka Wakuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa Mikoa na Waendesha Mashtaka wa Mikoa, kushiriki katika zoezi la uelimishaji Wananchi kuhusu usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari katika kipindi hiki cha msamaha.

Mlay ametoa rai hiyo hii leo Oktoba 1, 2023 wakati wa Kikao cha Menejimenti ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kinachoendelea Jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha udhibiti wa Silaha haramu wa Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kamishna Msaidizi wa Polisi, Berthaneema Mlay.

Amesema, zoezi hilo la usalimishaji wa silaha haramu linaendelea na litafikia tamati Oktoba 31, 2023 hivyo Wakuu hai wana wajibu wa kuendelea kuhamasisha Wananchi kushiriki kikamilifu, kwani silaha haramu zina madhara makubwa zinapotumiwa vibaya.

Katuka kikao hicho, pia Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamdun aliwataka Wakuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wa Mikoa, Wakuu wa Upelelezi wa Mikoa, na Waendesha Mashtaka wa Mikoa kujenga utamaduni wa kushirikiana, ili kazi ya upatikanaji wa haki iweze kuendelea zaidi.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 2, 2023
CCM yawapa majukumu mapya Jokate, Lulandala