Dereva wa mbio za magari ya langa langa wa timu ya Mercedes mwingereza, Lewis Hamilton amefanikiwa kushinda taji la nne la dunia katika michuano ya Mexico grand prix.

Hamilton aligongana na Sebastian Vettel wakati walipokuwa wakijaribu kupishana katika kona mwanzoni kabisa mwa mbio hizo za magari lakini alijitahidi kurudi na kufanikiwa kushinda taji hilo huku Sebastian Vettel ambaye ni dereva wa Ferrari akimaliza katika nafasi ya nne.

Mafanikio ya Hamilton yanamfanya kuwa dereva wa Uingereza ambaye amefanikiwa zaidi katika historia akiwa mashindano ya langa langa akiwa amevunja rekodi ya Jackie Stewart.

Hamiliton Anaungana na Vettel na mfaransa Alain Prost ambao wote wana vikombe vinne.

 

Serikali yataifisha kundi la ng'ombe kutoka Rwanda
Magazeti ya Tanzania leo Oktoba 30, 2017