Klabu ya Ruvu Shooting inasikitishwa na kitendo cha timu ya Toto ya Mwanza kumrubuni na kumsainisha mkataba kinyume cha sheria mchezaji wake Hamis Seleman.

Hamis Selemani ni mchezaji halali wa Ruvu Shooting na ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na kuwasilishwa TFF.

Ruvu shooting imemlipa mshahara kipindi chote hata mwezi uliopita akiwa likizo alitumiwa mshahara wake akaupokea kumbe tayari akiwa akiwa amesainishwa mkataba kinyemela na Toto bila uongozi wa Ruvu shooting kujua.

Ruvu shooting tunaomba klabu ya Toto imuachie mchezaji wetu ama kama inamhitaji uongozi uje tuzungumze, tukubaliane vinginevyo barua ya pingamizi tuliokwishaiandaa, muda ukifika tutaiwasilisha sehemu husika.

Hii itamweka pabaya kijana kwa kuwa na mikataba na timu mbili.

Otamendi Huyooooo Man City
BASATA Yalitoa Kifungoni Shindano La ‘Miss Tanzania’