Mwanamitindo maarufu, Hamisa Mobetto na Mchezaji nyota wa kimataifa wa mpira wa miguu Mbwana Ally Samatta wameteuliwa kuwa miongoni mwa mabalozi wa kuhamasisha ulipaji kodi nchini Tanzania.

Uteuzi huo umefanywa na Waziri wa Fedha na Mipango nchini, Dkt. Mwigulu Nchemba leo Juni 22 2021 Bungeni Dodoma ambapo mbali na wawili hao pia Mchambuzi wa mpira wa miguu, Mtangazaji Edo Kumwembe ameteuliwa.

Mbali na hao watatu kutoka kwenye tasnia ya michezo na Burudani, amewateua wanasiasa wengine kuwa mabalozi wa elimu ya kodi, ili kuhakikisha wananchi wanalipa kodi bila kushurutishwa.

”Vijana wanalugha wanazoelewana wao wenyewe kwahiyo kwenye kundi hilo nateua mabalozi wa kuhamasisha kulipa kodi kwa hiari, namteua Mbwana Sammata, Edoku Mwembe na Mwanamitindo Hamisa Mobetto” Amesema Dkt. Nchemba.

Chris Brown kuchunguzwa na Polisi
Diamond, Zari kuonekana Netflix