August 2016, Mbunge wa Handeni mjini, Omary Kigoda alieleza juu ya mabilioni ya fedha yaliyotengwa katika kushughulikia tatizo la maji wilayani humo, ambapo alitaja sh1.13 bilioni tayari zipo kuanza rasmi kutatua tatizo hilo.
Ambapo Mkuu wa Wilaya, Godwin Gondwe aliisisitizia mamlaka ya maji Handeni (HUWASA), na kuagiza maboresho ya huduma hiyo, lakini bado hali si shwari wilayani hapo.
Wananchi wanashangazwa kwani yapita mwaka sasa tangu fedha hizo zitengwe na Huwasa kuachiwa maagizo na mkuu wa wilaya kufanya maboresho ya huduma ya maji.
Hivyo wananchi wanahoji jitihada za mradi huo katika kutatua shida ya maji wilayani hapo, kwani imekuwa kero kubwa isiyozoeleka, kutokana na umbali mkubwa wanaoutumia kutafuta maji katika mabwawa na vijiji vya jirani.
Mmoja ya mkazi amezungumza amesema ”Tunaamka saa kumi kutafuta maji, lakini hadi kupata ndoo chache imefika saa mbili muda mwingine inafika hadi saa sita mchana kupata maji yakutosha kukidhi mahitaji ya familia”.
Baadhi ya wananchi wanadai kuwa uongozi uliopo wilaya ya Handeni ni uongozi ambao haujali maslahi ya wananchi, zaidi unaangalia masalahi binafsi.
Ni eneo moja tu ‘kwachaga’ ambalo lilibahatika kuchimbiwa kisima kutokana na shughili za utengenezaji wa barabara, lakini pia hiyo ilikuwa kama fursa kwa vijiji jirani kupata maji kama vijiji vya Amani na Mazingara lakini viongozi wameshindwa kufanya jitihada kuvuta maji hayo na kuyaleta katika vijiji vyao.
Sauti ya Dar24 ipae kwa viongozi husika kulishughulikia swala hilo ili wakazi hao kuondokana na shida ya maji kwani maji ni afya.