Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC Zacharia Hans Poppe ameibuka na kuonesha kuchukizwa na kauli ya Haji Manara ya kulipwa Shilingi laki saba kwa mwezi.

Manara alitoa kauli hiyo alipokua akimtuhumu Afisa Mtendaji Mkuu Simba SC Barbara Gonzalez usiku wa kumakia leo.

Hans Pope amesema Manara hakupaswa kusema upande wa kulipwa Shilingi Laki Saba pekee, bali alipaswa kusema na suala la kugoma kusaini mkataba ambao utafanya alipwe Shilingi Milioni 4 kwa mwezi.

Amesema kuna mambo mengi ambayo yanamzuia Manara kusaini mkataba huo, ambayo yatamuingiza matatani dhidi ya Kampuni ya GSM.

“Analalamika analipwa mshahara laki saba mbona hasemi kuna Mkataba wa Sh Milioni 4 hataki kuusaini hadi leo? Anajua utamfunga na atakuwa hawatumikii hao GSM” amesema Hans Poppe.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 23, 2021
PICHA: Simba yawasili salama Kigoma