Wakati kikosi cha Simba SC kinaondoka leo kwenda Zanzibar kuweka kambi, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe amewaambia mahasimu, Yanga SC wasubiri supu ya mawe kwa kachumbari ya pilipili manga na tomato Jumamosi wiki hii.

Mahasimu, Simba inayofundishwa na Muingereza Dylan Kerr na Yanga ya Mholanzi, Hans van der Pluijm ambayo tayari ipo kisiwani Pemba tangu jana, watamenyana wikiendi hii katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, timu zote zikitoka kushinda mechi tatu za awali.

Yanga imezifunga Coastal Union 2-0, Prisons 3-0 na JKT Ruvu 4-1 juzi, wakati Simba SC imezifunga 1-0 African Sports, 2-0 Mgambo na jana 3-1 Kagera Sugar.

Na Hans Poppe amesema baada ya ushindi wa 3-1 jana sasa wanakwenda kambini Zanzibar kuiandalia Yanga SC ‘dozi nene’ na amewataka wapinzani wao hao wa jadi wakae tayari.

“Yanga SC wanapiga sana kelele, imekuwa timu ya magazetini, inasifiwa sana wakati uwanjani haina lolote. Sasa wasubiri supu ya mawe iliyochanganywa na kachumbari, pilipili manga na tomato Jumamosi,”amesema.

Mabasi Mengine 138 Ya Mwendo Kasi Yashushwa Dar
Kumuona ‘Live’ Mtoto Wa Diamond Utalipa Shilingi Ngapi?