Serikali imeridhia ombi la kujengwa kwa Mnara wa Sokoine katika eneo la Dakawa mkoani Morogoro, eneo alilopata ajali na kufariki dunia Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

Ridhaa hiyo imetangazwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango wakati akifungua mdahalo wa kumbukizi ya Hayati Sokoine kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro.

Dkt. Mpango ameridhia ombi hilo ambalo awali lilitolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako.

Makamu wa Rais amemuelekeza Profesa Ndalichako kushughulikia mchakato utakaofanikisha kujengwa kwa Mnara huo wa Sokoine, aliyefariki dunia mwezi Aprili mwaka 1984.

Hoja darasa la saba kukosa ajira serikalini yaibuliwa bungeni
Biden ataka chanzo cha corona kuchunguzwa upya